Kuelekea mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya kagera sugar na Geita Gold utakao pigwa leo jijini mwanza katika uwanja wa CCM kirumba majira ya saa kumi jioni, Kagera Sugar ambao ni wageni katika mchezo huo wamesema kuwa wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata ushindi.
Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo Hamis Kiza moja ya wachezaji wa kagera sugar amesema kuwa licha ya kupoteza michezo miwili tangu kuanza kwa ligi kuu wao kama Wachezaji kwa kushirikiana na mwalimu wao wamejipanga upya kuhakikisha wana pata matokeo kwenye mchezo wa leo na mingine iliyo mbele yao.
MATOKEO YA KAGERA SUGAR NA GEITA GOLD
Zaidi amesema kuwa jambo kubwa ambalo wamelikusudia ni kufanya mashambulizi kwa tahadhari ya kulinda mashambulizi kutoka timu pinzani.
Hadi hivi sasa Kagera sugar wanashikirilia mkia kwa kupoteza michezo yote miwili kati ya Azam Fc na Simba Sc wakifuatiwa na Dodoma Jiji pamoja na Ihefu.